TECNO YAWAPONGEZA WASHINDI WA SPARK.




Kampuni ya TECNO imeonesha ni kwa jinsi gani inathamini wateja wake kwa kuaandalia hafla maalumu  kuwapongeza wateja  wa simu mpya ya TECNO SPARK. 
Timu  ya TECNO ikiwa  tayari kwa hafla maalumu jijini Mwanza.

TECNO inayofanya kampeni ya simu mpya iliyopatia umaarufu mkubwa nchini TECNO SPARK imewaandalia wateja wake hafla ya maalumu ya kuwashukuru  kwa kuwaunga mkono pamoja na kuwapa zawadi za  aina mbalimbali ikiwemo simu mpya  ya TECNO SPARK iliyokwenda kwa mshinid bwana Baraka Modo mkazi wa Mwanza. 
Mshindi wa SPARK Bwana, Baraka Modo akikabidhiwa zawadi yake na timu ya mauzo ya TECNO mkoani Mwanza

Akizungumza wakati wa hafla  hiyo ,Afisa Mahusiano wa TECNO bwana , Eric Mkomoye amesema kwamba TECNO inaendeleza utaratibu wake wa kuwajali wateja wake kupitia  matukio mbalimbali yatakayokua yanaandaliwa kwa nia ya kuwapongeza wateja wa TECNO na kuwaweka karibu na kampuni hiyo kama ambavyo mteja wao katika hafla hiyo bwana  Baraka Modo alivyojishindia TECNO SPARK. 

Wateja wa Tecno mkoani Mwanza  walipata nafasi ya kuingia kwenye hafla hiyo maalumu iliyoitwa TECNO BLUENIGHT baada ya kununua simu ya TECNO SPARK, huku wengine wakipata tiketi kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO.

TECNO inaendelea kuwahimiza wateja wake kujumuika katika kampeni mbalimbali inazoziendesha ili  wateja waweze kufaidika zaidi. 

Simu iliyowezesha wateja hao kuwepo katika hafla hiyo maalumu ni TECNO SPARK simu mpya iliyojipatia umaarufu mkubwa nchini kwa umbo lake la kuvutia, ikiwa ina usalama wa alama za vidole (finger print), kioo chake ni kikubwa huku ikiwa na camera ya 13mp nyuma na 16gb za kuweka data za aina zote katika simu bila kutumia kadi kumbukumbu (Memory kadi). 



Post a Comment

0 Comments