TECNO YA MANCHESTER CITY HII HAPA.



Tecno Mobile imetoa simu bomba kwa ushirikiano na klabu ya mpira  ya Manchester  city na simu hii ni inasifika kwa umbo zuri sana.
Simu nyingi zimekua zikitengenezwa kwa umbo la plastiki haijalishi maumbo yao lakini kinachotengenezewa ni plastiki lakini kwa miaka ya hivi karibuni maumbo yamebadilika kutoka plastiki mpaka metali na glasi. Simu zilizotengenezwa kwa metali ni simu zinazoonekana za juu na zenye thamani Zaidi.
Simu hii ya Manchester city imetengenezwa kwa metali hivyo ni simu imara  na inayoenda na wakati. 




Katika kuhakikisha simu hii inakua n aumbo na ubora unaotakiwa katika na soko, simu hii Tecno Camon CX tolea maalumu ya Manchester City Inakuja ikiwa na vitu vingi adimu hasa katika muonekano wake.
Tolea maalum la  simu hii awali ya yote itakua na  alama ya timu ya Manchester City nyuma kwa chini ili kuleta  ladha ya klabu hiyo mikononi mwa watumiaji. Huku kioo cha simu hii kina ukubwa wan chi 5.5  FHD Inayotoa nafasi kwa mtumiaji kuangalia video vizuri kabisa, mteja wa Tecno Mobile akiishika simu hii sio tu kwamba itampa  `ujasiri wa kuonyesha  mbele za watu bali pia raha ya kuitumia.


Tecno imeamua kufanya makubwa  kwa wateja wake na kwa muonekano wa simu hii inadhihirisha kwa kiasi gani wateja wake watafaidika, simu hii imara inabeba  kamera yenye 16MP mbele na nyuma wakati kwa upande wa mwanga simu hii ibebwa na LED flashi mbele zikiwa mbili huku nyuma zikiwa nne katika mfumo wa ringi. 


Uwezo wake wa  kuprosesi data ni 4GB na 64 GB ikiwa ni uwezo wa kuweka vitu kwa ndani, simu hii mteja anaweza kuongeza kumbukumbu pia kumbuka mfumo wake ni wa android 7.


Having a device as strong and beautiful as this in this modern day for a price that is reportedly affordable is only synonymous to a steal.
Kua na hii sio simu sio tu ni furaha kwao ila inakufanya uweze kwenda na wakati kwa price  unayoweza kuimudu.



Post a Comment

0 Comments