Kampuni
ya simu ya Tecno Mobile iliyoingia makubaliano ya kibiashara na Timu maarufu
inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu
nchini Uingereza Klabu ya Manchester City, kwa pamoja wamekuja na mikakati ya
kukuza soka nchini Tanzania.
Kwa
Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na
Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Bwana
Eric Mkomoye, amesema kua pamoja na kuwapo kwa fursa za kibiashara zilizopo
kati ya klabu ya Manchester City na Tecno Mobile lakin pia Tecno wamedhamiria
kutumia fursa hiyo kukuza viwango vya mpira kwa watoto wa
kitanzania ambao wazazi wao pia ni wateja wa kampuni hiyo
“Tutawapa
watoto wa kitanzania kadhaa nafasi ya kwenda Manchester city kufanya training
kule na pia wakifanya vizuri wanauwezo wa kuchukuliwa kwa academy ya Manchester
City , huko watakutana watoto wengine tokea nchi ambazo Tecno Mobile inafanya kazi zake kama Kenya, Uganda, Ghana na Misri na kwa
kuanza tutapeleka watoto wawili”
Katika
ushirikiano huu pia imeleta simu maalumu itakayotumika alama maalumu ya
Tecno Mobile na klabu ya Manchester
City, Eric alifafanua.
“Tumeleta
Tecno Camon CX Manchester city limited
version, ni simu maalumu inayoonesha ushirikiano wetu na Man city pia ni simu maalumu inayotumika wachezaji wa
Manchester city katika kupiga picha , hivyo tumeileta sokoni maalumu kwa
wateja wetu kipindi waweze kupata
experience wanayopata man city katika
simu hii.”
Aliongeza “Simu hii inakuja na box kubwa lenye zawadi maalumu kwa wateja kama chupa ya kimichezo, speaker, fimbo maalumu ya kupigia picha pamoja na kava maalumu.”
TECNO
Mobile wameleta simu ikiwa ni toleo maalumu la tecno camon cx iliyokua sokoni
mapema kidogo ila limeboreshwa Zaidi, hivyo inaenda na wakati uwezo wa kamera
yake ni 16mp nyuma na mbele zinazosaidiwa na flashi mbili mbele nanne nyuma,
uwezo wake ndani ni 64 GB huku ikisukuma data vizuri kwa 4GB Ram,
Watoto
watakaochaguliwa na Tecno Mobile kwenda
katika trining hiyo wanatarajiwa kuondoka nchini mwisho wa mwezi nane, na
vigezo vikubwa Tecno imetumia wataalamu wa soka nchini kutafuta vipaji hivi,
Majina ya watoto hawa yatatangazwa kupitia mitandao ya kijamii ya Tecno Mobile.
0 Comments