Msechu akiri kuwa yeye si mwandishi mzuri, afungua milango kwa yeyote kumwandikia nyimbo zake

Msechu
Msechu akiri kuwa yeye si mwandishi mzuri, afungua milango kwa yeyote kumwandikia nyimbo zake
By star_king_worldwide
Peter Msechu ni miongoni mwa wasanii wachache ambao hawaoni shida kukiri kuwa si wazuri kwenye upande wa uandishi wa nyimbo, licha ya kuwa na kipaji na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza vyombo vya muziki.
Msechu
Baadhi ya wasanii (wa Bongo) huwa hawapendi kusema ukweli pale wanapoandikiwa nyimbo na wasanii wengine, kwa kudhani watu wakijua wameandikiwa inaweza kuwapunguzia thamani.
Msechu ambaye ameachia wimbo mpya wiki iliyopita, amesema kuwa baada ya kugundua kuwa sio mzuri kwenye upande wa uandishi wa nyimbo, sasa hivi nyimbo zote atakazorekodi atakuwa anawapa watu wengine kazi ya kuandika na kumpa njia na sauti ya kuimbia (melody).
“Unajua nimekuja kugundua kuwa nilikua sijitambui, nilikua nalazimisha kuandika nyimbo kitu ambacho nilikuja kugundua kuwa mimi sio mzuri upande huo.” Alisema Msechu kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.
Msechu aliongeza kuwa wimbo wake ‘Nyota’ ambao wote aliandikiwa na Amini ndio umetokea kuwa wimbo mkubwa na uliompa mafanikio kuliko nyimbo zote alizowahi kufanya.
‘Nyota’ ndio wimbo ambao pia ulimpa nafasi Msechu ya kutajwa kuwania tuzo za Kimataifa za AFRIMA 2014 za Nigeria kwa mara ya kwanza.
Wimbo mpya alioutambulisha wiki iliyopita ‘Malava; umeandikwa na Barnaba. Msechu amefungua milango kwa msanii au mwandishi yeyote anayehitaji kumwandikia nyimbo yupo tayari kufanya naye kazi.

Imetayarishwa na @star_king_worldwide na www.wasaportz.blogspot.com
&Tunersproduction
Follow us on instagram
@star_king_worldwide                                      
@wasaport_tz
@tunersproduction

Email


                                         *****@2015******

Post a Comment

0 Comments