Mwanamuziki wa Muziki wa Hip Hop, Sarah Hopah Kimario ‘Sarah Kim’ ameibuka na kusema kwamba ngoma yake mpya ya Break Up Day ndiyo iliyomuumiza kichwa chake katika kipindi alichokuwa akiitunga.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Sarah alifunguka kuwa wakati alipopata wazo la kutunga wimbo huo, ilimuwia vigumu sana lakini mwisho wa siku aliweza kuibuka na kitu kikali kilichomfanya kusikika masikioni mwa watu wengi. Kwake, haikuwa rahisi, ilimuwia vigumu sana mpaka kukamilika kwa wimbo huo.
“Nilipata wakati mgumu sana,” alisema Sarah na kuongezea:
“Sikuamini kama ningeweza kuandika wimbo mkali kama huu. Nilipata wakati mgumu sana, niliandika mistari, nikafuta, yaani kila idea iliyokuja kichwani niliiona kutokufaa ila mwisho wa siku, nikatunga wimbo huu” alisema Sarah.
Sarah ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa pili anayechukua kozi ya Computer Engineering. Kwa sasa, ngoma zake zote anazifanyia katika Studio ya Tunes Production chini ya Prodyuza Eddy Lesser.
4 Comments
Iko poa
ReplyDeleteEti nasikia Melody yule wa Toto party atarudi upya mwaka 2016 kupitia tuners production napenda kuuliza vp ni kweli na je amesharekodi nyimbo zp tuners
ReplyDeleteEti nasikia Melody yule wa Toto party atarudi upya mwaka 2016 kupitia tuners production napenda kuuliza vp ni kweli na je amesharekodi nyimbo zp tuners
ReplyDeleteHuyu Dada Sarah ananikumbusha Enzi za rah p kipndi kwenye ushindani na sister p anaswag nzuri namtakia kila lakher swali LA kizushi vp anamchumba mm nimetoka kumpenda Sana uyo dada
ReplyDelete